Jinsi Ya Kumsaidia Mtoto Mchanga Kupata Haja Kubwa

Kukosa choo kwa watoto wachanga(constipation) ni kawaida, sababu utumbo haujazoea kupokea chakula bado.Mtoto anaweza kosa choo kwa siku 3-7. watoto wengi hupata tatizo la kukosa choo pale wanapoanza kula vyakula vigumu(solid food) wakiwa na miezi 6. Iwapo akakosa choo kwa mda mrefu zaidi mpeleke hospital watamsadia.

  Jinsi ya kumsaidia mtoto aliekosa kupata haja kubwa

  •  Watoto walio chini ya miezi 6 wanaweza fanyiwa massage kuanzia tumboni juu kuja chini kwa kutumia mafuta ya maji taratibu, inasaidia kusukuma kinyesi kwa urahisi na baada ya mda atapata choo.colico51

Kwa watoto walio juu ya miezi 6 wanaweza pewa

  • Maji apewe  mara kwa mara itamsaidia kulainisha tumbo.

  • Matunda apewe tofauti tofauti mara 2-3 kwa siku yanayosaidia kulainisha tumbo Ili kupata choo kwa urahisi kama papai,parachichi,machungwa,peach,prunes,apple,embe n.k

  •  Mboga za majani apewe kila siku, sababu zina nyuzi nyuzi (fiber) zinazosaidia mmeng’enyo wa chakula kuwa rahisi, mboga za majani kama spinach, mchicha ️au kabichi.Unknown

  • Mtindi -mtoto mwenye umri wa miezi 8 na kuendelea anaweza pewa mtindi unasaidia kulainisha choo

  • Mama unatakiwa kunyonyesha mtoto kwa wingi itamsaidia kupata choo kwa urahisi.

NOTE: Kabla hajapata choo jaribu kumpaka mafuta ya Vaseline au olive oil kwa nje ya njia ya haja kubwa kumsaidia asipate maumivu makali akipata choo.

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →