Ni Mda Gani Mzuri Mtoto Kulalia Tumbo?

Ili kupunguza vifo vya mtoto mchanga wataalamu wanashauri kwamba mtoto mchanga unatakiwa kumlaza kimgongo mgongo kwa kipindi cha mwaka wake wa kwanza kwa sababu kipindi ambacho anaweza kupatwa na maafa kipindi ambacho yupo hatarini sana ni kuanzia akiwa na umri wa mwezi mmoja hadi minne 1-4, ila bado anakua kwenye hatari mpaka atakapofikisha umri wa miezi 12.

 

Mtoto wako akianza kujizungusha zungusha kuanzia kulalia mgongo na tumbo basi unaweza kuondoa hofu kama akilalia tumbo akiwa usingizini.

 

Baadhi ya Hatua unazoweza kuchukua ili kupunguza vifo vya mtoto ni kama

 

– Hakikisha kitanda cha mtoto kipo safi

– Hakikisha kitanda hakijajaa vitu na kuzungukwa na vitu kama midori, mito mpaka akakosa hewa

– Usimvalishe nguo nyingi wakati wa kulala, avae nguo laini tuu labda kama ni maeneo ya baridi

– Hakikisha hamna mtu anaevuta sigara karibu yake

– Muweke sehemu ambayo haina joto sana na hakikisha mazingira ya mtoto sio ya hali ya joto

 

Kwahiyo kwa kifupi tena, ni vema mtoto wako akianza kulalia tumbo akishafikisha umri wa mwaka mmoja hapo  inakua haina matatizo yoyote, ila vile vile ni wewe kama mzazi kumwangalia kweli akilalia tumbo anakuwa kawaida au anakua hana amani, kama ukiona bado anakua hana amani basi muache mpaka pale atakapokuwa na amani pindi alaliapo tumbo.

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →