Mtoto Wangu Anapenda Kubebwa Mda Wote. Kwa nini?

Je mtoto wako anapenda kubebwa mda wote?…well hauko peke yako maana hawa  watoto wetu  wakiwa bado ni wadogo sema kweli huwa wana mambo sana iwe wa kike au wa kiume. Kuna hii tabia yakuwa anapenda kubebwa mda wote kila mara  jamani sijui kama imeshawahi kukuta. Kama bado huna mtoto jiandae maana ni balaa.

 

Unakuta mtoto analia hapo unampa maziwa na kumyonyesha anakunywa vizuri kabisa bila shida yoyote na ametulia mpaka anashiba, we si unajua ametulia  kumbe njaa ilikua ina msumbua sasa unamuweka chini hapo, yaani hata kabla hujafika jikoni kilio kitakachokufata hapo nyuma mama yangu weeeeee alafu ukirudi kumbeba tu huyooo anatulia tena na anakuchekea kabisa.

 

Yaaani me mwenyewe najua jinsi inavyokera maana unakuta unataka kupika chakula af yeye anaanzisha biashara ya kulia na ukuta akina mama wengine wanaamua kabisa kumuacha aliee weee mpaka alale. So kwanini huyu mtoto wako anapenda kubebwa mda wote?

Anapenda Kubebwa Mda Wote

Well  iko hivi mtoto ambaye ana miezi 2 mpaka 4 au 5 huwa anaanza kujua kujua na kuwa na mkanganyiko  kuwa yeye ni mtu tofauti na mama yake, na kwa sababu ameanza kujua hilo kuwa yeye anaweza kuwa peke yake bila mama sasa anaanza kuwa na woga kuwa ukiondoka huwezi kurudi. Yaani anajua ukiondoka huwezi kurudi. Sasa mbaya zaidi ni kwamba mtoto mdogo wa umri huo miezi 2 mpaka 4 au 5 huwa bado hawana kumbukumbu ya kutosha kwa hiyo hakumbuki kuwa mara ya mwisho ulivyoondoka ulirudi yeye anajua tu ukiondoka ndio kimoja haurudi ndio maana Kilio atakachokitoa hapo ni balaa. Kwa hiyo wanalia kwa sababu wanakua bado wanakuhitaji. Hii huwa inakua hivi kwa miezi 2  mpaka 3 ya mwanzo.

Kwa hiyo unashauriwa kabisa mtoto akiwa analia pale ni vema ukambebaa mbembeleze wee hapo mpaka alale zake maana ukimuacha alie kwa kweli unakua unamuonea maana mwenzio anajua wewe ndio unaondoka na hauna mpango wa kurudi, kwa hiyo  ili kuwekana sawa ni vema ukaendelea kumbembeleza ili asiendelee kulia na kupoteza maji mwilini.

 

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →