Mtoto Anatakiwa Kunyonyeshwa Kwa Kiwango Gani?

Mtoto mchanga  alie chini ya miezi sita anahitaji kunyonya kila baada ya masaa 1-3 kulingana na mahitaji yake.Mwezi wa kwanza wa mtoto ananyonya maasaa 8-12 kwa siku,watoto walioanza kula vyakulakuanzia miezi 6 kiwango cha kunyonya kinapungua sababu anakuwa anakula chakula kizito atanyonya mara 4-5 kwa siku inategemeana na mtoto na mama wengine inaweza kuwa zaidi ya hapo. Mama unapohisi huna maziwa ya kutosha hutakiwi kupanic chamana kula vizuri na mwachwe anyonye sababu kila anyonyapo anachochea maziwa kutoka  kwa wingi.

 

image

Utajuaje mtoto akiwa na njaa.

Mtoto anapokuwa na njaa ndio mda sahihi wa kunyonyesha,ila mama zingatia mda kama ulimnyonyesha saa 4 ikafika mida ya saa 6-7 hapo lazima atakuwa na njaa ,ni vizuri umpe kabla hajaanza kulia mana akilia sana mtashindwa kunyonyesha na utapata stress.

dalili za mtoto mwenye njaa

 • Kuzungusha kichwa kila upande

 • Kunyonya vidole

 • Kunyonya midomo na kuonyonya kama anataka nyonya nyonyo

anaweza onyesha ishara hizi akiwa  analia au bila kulia.

 

ANGALIA LIA HIZI PICHA UTAMBUA DALILI ZA NJAA KWA MTOTO
ANGALIA LIA HIZI PICHA UTAMBUA DALILI ZA NJAA KWA MTOTO

Mtoto anatakiwa kunyonyweshwa kwa muda wa dakika 20 kwa kila ziwa moja kwa jumla ni dakika 40 kwa watoto wachanga,Kadiri mtoto anavyokuwa muda unapungua  kunyonya  wanakuwa dakika 10-15 kwa kila ziwa.Mama unatakiwa umweke mtoto vizuri ili aweze kumudu kunyonya vizuri hakikisha mdomo wake wote umeingia ndani ya chuchu,ufunike ule duara jeusi wa kwenye ziwa ,

image
HII NDIO NJIA SAHIHI YA MTOTO KUNYONYA,LIPS KUFUNIKA DUARA JEUSI

asivute chuchu kwa nje bila lips zake kuingia ndani ya duara jeusi,usipofanya hivyo maziwa hayata mfikia ipasavyo na  utachubuka kwenye chuchu na kupata vidonda kwenye  chuchu yenye kuleta maumivu makali.

 

Tiba ya vidonda /mchubuko kwenye chuchu

Unapopata vidonda kwenye chuchu unaweza tumia

 

 • Mafuta ya nazi au olive oil  pasha yapate moto kidogo na fanya kama massage kwenye kidonda  mara 4-5 kwa siku,itasaidia kulainisha ngozi kutoa ile ukakamavu.

 • Dawa ya kupaka unaweza pata dawa maduka ya dawa.

 • Barafu-chukua kipande cha barafu wekea kitambaa funika na jiweke kwenye chuchu kwa dk 5-10 fanya mara 4-5 kwa siku

 • Paka maziwa yako kwenye chuchu baada na kabla ya kunyonyesha

 • Basil (mrehani)ponda ponda na upake chenye chuchu ,safisha vizuri kabla ya kumnyonyesha mtoto.

CHUCHU YENYE KIDONDA
CHUCHU YENYE KIDONDA

Utajuaje mtoto ameshiba

 • Utamwona karidhika na hasumbui

 • Diaper au nepi yake itajaa kwa haraka sana(anatatumia diaper 6-8 kwa siku)

 • Atalala vizuri kwa masaa ya kutosha baada ya kunyonya

 • Kuongezea uzito

 • Kupata choo mara 2-3 kwa siku

 

 

 

Mtoto asieshiba anadalili hizi

 • Kuto kuongezeka uzito

 • Kulia mara kwa mara

 • Diaper au nepi inachukua mda kujaa

 • Kuhisi njaa baada ya mda mfupi

 • Matiti kuto kujaa,kutokuvuja

Unapoona mtoto hataki kunyonya ndani ya msaa 24-48 ujue kuna tatizo mpeleke hospital au kuna vyakula unakula vinavyozalisha gesi kwake na kumfanya muumiza tumbo kama chocolate,kahawa,red bull,cocacola,broccoli,kabichi,pombe na maziwa ya nido.

 

image

 

Watoto wengine wanashiba mapema wanachukua dakika 10-15 kwa kila ziwa badala ya 15-20.Mama unaponyonyesha inatakiwa unyonyeshe maziwa yote mawili kwa muda sawa kama ni dakika 15 -20 usije nyonyesha ziwa moja kwa wingi kuliko jingine ,hilo usilo nyonyesha litakuwa dogo na hilo jingine litakuwa kubwa kiasi cha kwamba ukiva nguo itaonyeshautofauti , mtoto hatolitaka kunyonya tena sababu maziwa yake yatakuwa yamechacha kutokana na kutonyonywa mara kwa mara,kila ukimnyonyesha atahisi machungu  na kukataa.

KUNA MIKAO TOFAUTI YA KUKAA WAKATI WA KUNYONYESHA MTOTO
KUNA MIKAO TOFAUTI YA KUKAA WAKATI WA KUNYONYESHA MTOTO

Hili tatizo linawapata wamama wengi kipindi cha usiku wanaponyonyesha wakiwa  wamejila kitandani na upande rahisi kunyonyesha ni wa kushoto ,na kujikuta kuto kunyonyesha upande wa kulia.

 

 

 

Mama kuhisi hana maziwa ya kutosha::

Wamama wengi wanawaza hawana maziwa ya kutosha hapana ni hisia zako tu maziwa yapo kinachotakiwa mnyonyeshe mtoto mara kwa mara kila anyonyapo ndio huchochea maziwa kutoka kwa haraka na kwa wingi ,mtoto alie chini ya miezi 6 haitaji kupewa chakula chochote zaida  ya maziwa ya mama ,unatakiwa kula lishe bora sio kula chips tu hapo lazima utakosa kuzalisha maziwa ,kunywa maji kwa wingi( na vimiminika vingine isipokua pombe) na jipe mda wa kupumzika hapo lazima maziwa yatatoka.

 

 

 

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →