Morning Sickness In Pregnancy

Wajawazito kupata hali ya kutojisikia vizuri kipindi cha asubuhi ni hali ya kawaida ,japo inakosesha raha kukufanya kunyong’onyea kutapika ,kupata kama homa kidogo,mate kujaa kinywaji,kichefuchefu.Hali hii inajitokeza kipindi cha miezi mitatu za mimba first trimester ambapo mama akifikisha wiki ya 4-6 hapo hali inaanza mwanzo.

Bulimic young african woman forcing herself to vomit

Japo sio wajawazito wote inawakuta inategemea kwa kila mtu.Kwanini mama anapata hiyo hali inasababishwa na nini? Morning sickness haina sababu ya moja kwa moja inayosababisha ila sababu kubwa ni ile hali ya mama kuwa mjamzito na kufanya mabadiliko ya mwili wake(kuzalishwa hormones kwa wingi ndipo anapata hali kama iyo .

 

  Morning sickness inasumbua sana mjamzito mwenye matatizo gani? 

Kuna group la mama wajawazito  wanaweza kapata morning sickness kwa kiwango kikubwa kwa sababu zifuatazo

 

1:Mjamzito mwenye mapacha

2:Mama anaeshikwa na morning sickness kila ashikapo mimba,anadalili ya hi hali kujirudia ashikapo mimba tena.

3.Mama kama alikuwa anatumia vidonge vya majira (uzazi) anaweza pata morning sickness kwa wingi

4.Mama anatatizo la kupata kipandauso (maumivu makali ya kichwa mpaka macho) inaweza pia msababishia morning sickness.

5.Mama akiwa na mimba ya mtoto wa kike-baadhi ya tafiti zinasema mama akiwa na mimba ya mtoto wa kike wanapata morning sickness kwa asiliamia flani.

 

Morning sickness haina madhara yoyote kwa mtoto unachotakiwa kuzingatia kutumia prenatal vitamins.

 

 

Njia za kupunguza morning sickness

 

Mama mjamzito anaweza kupunguza hali mbaya anayojisikia kwa kukwepa haya yafuatayo

1:Epuka kula chakula kingi kwa pamoja ,kula portion ndogo ndogo.

2:Epuka kulalia ubavu baada ya kula haswa upande wa kushoto itasababisha chakula kusagwa taratibu sana

3.Epuka vyakula vya harufu kali au perfumes ambazo unaona zinakukchefua.

4:Kula chakula cha baridi au chenye joto la mbali

5:Epuka vyakula vya mafuta mengi ni ngumu kusagika kwa urahisi na itakuchefua

6:Kunywa vimiminika wakati wa kula

7:Epuka kunywa vimiminika wakati unajihisi tumbo limejaa(kkushiba)

8.Unapotapika jaribu kunywa kinywaji cha kukupa nguvu chenye glucose,chumvi

9.Piga mswaki kila baada ya mlo.

10.Toka nje tembe upate fresh air

11:Tafuna tangawizi au weka kwenye chai kamulia na ndimu kunywa.

 

images

 

 

12:Kunywa maji ya kutosha,epuka kuwa hydrate

13.Weka ndimu kwenye maji vugu vugu kunywa

14.,Tafuna majani ya minti ,kula machungwa

15:Tumia vidonge vya prenatal vitamins

16:Jipe mda wa kupumzika (kulala)

17:Epuka kulala kwa mda mrefu fanya mazoezi

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →