Mimba Miezi 8:Ukuaji Wa Mtoto Na Mabadiliko Ya Mwili Wa Mama

Hongera mama kwa kufikisha miezi 8 (wiki 32) umebakiza mwezi mmoja ujifungue.Mtoto ameshakuwa mkubwa na uzito umeongezeka mama na kuelemewa wakti mwingine ,mabadiliko ya mtoto ni

 

 

Mimba ya miezi Nane

 

 

 • Uzito wa mtoto ni 2kg au 2.5g
 • Urefu wa mtoto ni inches 16-17
 • Kila mtoto alalapo analala kwa muda wa dakika 20-40
 • Viungo vya mtoto bado vinaendelea kukua na kukomaa lishe bora ni muhimu kwa mama ili kusupport ukuaji wa mtoto.
 • Kichwa kimegeuka na kuangalia chini tayari kusubiri kutoka ,kwa mara nyingi kichwa kitakuwa chini mpaka mda wa kujifungua utakapo fika,japo kuna wakati wanajigeuza na baadhi ya hospital watakusaidia kumgeuza kwani ni hatari mtoto kugeuza kichwa kuangalia juu kwa miezi ya 8-9,iwapo mama akashikwa uchungu mtoto anaweza tanguliza mkono,miguu badala ya kichwa ni ni hatari,mtoto anauwezo wa kujigeuza pia mwenyewe bila msaada wa hospital.
 • Mtoto anauwezo wa kusikia sauti za nje za watu wakiongea au music

 

Mabadiliko ya mama

 • Kutanuka kwa njia ya uzazi ,utasikia ukeni panavuta vuta na maumivu ya kuja na kuondoka
 • Kupata tabu ya kupumua ,mtoto anakubana sana haswa sehemu ya mbavu na upumuaji wako unakuwa mgumu
 • Mafua ya kudumu (sio kwa wote)
 • Matiti kuanza kuvuja maziwa
 • Kuchoka kwa mama kunaongezeaka
 • Kutokwa maji maji ukeni
 • Kiungulia (heartburn)
 • Maumivu ya mgongo
 • Mama anakojoa mara kwa mara
 • Tumboni kwa mama utapata mstari mweusi toka juu kuja chini unaitwa Linea nigra
 • Kulala kwa tabu usiku

 

Ushauri

Endelea na mazoezi ya kuogelea,kutembea,stretching ,yoga n.k epuka kubeba vitu vizito,kuruka kamba au kukimbia ni hatari kichwa cha mtoto kinaangalia chini kwa sasa.Mama unaweza fanya shopping ya mtoto ,na kuanza kuapack bag utakalo enda nalo hospital siku ya kujifungua,fatilia posts zijazo utaona list ya vitu unavyotakiwa kubeba.

 

Ukaona dalili hizi wahi hospital

 

 • kuvimba miguu,mikono,kizunguzungu
 • Kuishiwa nguvu,kutokwa maji mengi ukeni ujue chupa imepasuka wahi hospital
 • Kuwashwa ukeni na kutokwa maji maji ya njano au meupe yenye harufu wahi hospital itakuwa infection,UTI au fungus
 • Pressure kupanda au kushuka,mwili kubadili rangi mikononi,miguuni,kucha n.k wahi hospital
 • Kutokwa damu nyingi,mtoto kuto kucheza.

 

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →