Mimba Miezi Saba:Mabadiliko Ya Mama Na Mtoto

Mimba miezi saba  (wiki 28-29) mama ameingia kwenye( third trimester ) miezi mitatu ya mwisho,safari inazidikuwa ngumu kwa kupata miwasho mingi tumboni (stretchmarks) zinajitokeza sasa kwa wingi na kuwasha sana ,epuka kujikuna na paka mafuta tumboni mara kwa mara hakikisha ngozi isiwe kavu.

mimba ya miezi saba

 • Mama anapata tabu kulala usiku na mikiki ya mtoto inakuwa mingi zaidi ,
 • kuongezeka uzito kwa mama -kunakufanya mwili uwe mzito na kuongeza kiasi cha kula kuwa kikubwa japo inategemea wengine wanapoteza hamu ya kula,
 • Matiti  kujaa baadhi ya wamama wanaanza tokwa maziwa
 • Kiungulia(heartburn)
 • Constipation (tatizo la kutopata ajakubwa)
 • Maumivu ya mgongo / chini ya kitovu chini ya tumbo
 • Miguu kuvimba kwa baadhi ya wajawazito

Mabadiliko ya mtoto

 • Mtoto amekuwa na kuongezeka urefu kuwa 36cm(14inches) na uzito kati ya 900-1800g,ubongo wa mtoto unakuwa kwa haraka kwa kipindi hiki,
 • anaanza kuona na kusikia sauti za nje ,
 • internal system zake zinakuwa ,mapafu na misuli  bado inaendelea kukua,
 • Kugeuza kichwa

Ushauri  Wa Afya Bora Kwa Mtoto

Mama umeona ukuaji wa mtoto bado unaendelea sasa unatakiwa kula mlo kamili wenye virutubisho vingi kama nyama,samaki,mboga za majani,matunda,maziwa,mtindi,mayai,viazi,wali ,ugali,kunde,choroko,njegere,

maji kunywa kwa wingi n.k ili kusupport ukuwaji wa mtoto,epuka kula vyakula vya fast food kama chips,pizza,burger n.k havina virutubisho vyovyote kwa mwili wako na mtoto.

Ukahisi dalili zozote usizozielewa mwone daktari mapema kwa usalama wako na mwanao.

 

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →