Mimba Miezi Sita :Ukuaji Wake,Mabadiliko Ya Mama Na Mtoto

Wiki ya 24 (miezi 6) ni second trimester tumbo la mama lishajitokeza kuwa kubwa kiasi cha kuonekana ,mtoto nae anazidi kukuwa amebakiza miezi 3 kuja duniani ,ameongezeka uzito na kuwa na 660g na urefu wa 35cm,anapata mabadiliko ya mwili kama

 

 

image

  • Kuanza kupumua kwa kidogo kidogo

  • Mtoto amekuwa mkubwa na ubongo unazidi kukua  hapo ni vizuri mama akala samaki kwa wingi na kutumia olive oil kwa chakula inasaidia kukuza ubongo.

  • Mishipa na mifupa inakuwa na kuanza kukomaa zaidi  kumfanya kuwa na movement nyingi kiasi cha mama kusikia akicheza tumboni

  • Ngozi yake bado inajitengeneza .

  • Anaweza kushika na kunyonya kidole chake

 

Mabadiliko kwa mama yanaweza ongezeka au asipate mabadiliko akabaki na yale ya wiki 20(miezi 5) sababu kila mama mjamzito na mabadiliko yake sio yakufanana ,iwapo  mama atapata mabadiliko wiki hii ya 24 ( miezi 6)

  • Uzito-mama ataongezeka uzito kwa kiasi flani

  • Joto-mwili wa mama utachemka ajasikia joto na kutokwa majasho

  • Moyo -mapigo ya moyo ya mama yataongezeka (yanapiga kwa haraka zaidi)

  • Maumivu kwenye mbavu-mtoto atakuwa anambana sana na kupumua kwa tabu

  • Kuvimba miguu-wa mama wengi wanaanza vimba miguu / uso kipindi hiki

image

Mama amebakisha miezi 3 kujifungua anawaza labour ipoje  siku ya kumwona mwanae akijifungua itakuwaje,kwenye hii wiki ya 24 wazazi wengi waanza kufanya shopping ya mtoto na kutafuta jina la mtoto kama ni wakike au kiume. Pima kiasi cha sukari mwili sababu kipindi hiki cha miezi 3 ya mwisho ndio tatizo la protein kwenye mkojo/ high blood pressure linapoanza kujitokeza ni hatari ka mama na mtoto unaweza pata kifafa cha mimba(preeclampsia)

 

USHAURI TOKA KWA AFYABORA……

Vaa viatu flat,fanya mazoezi ya kutembea,kuogelea,stretching,Yoga epuka mazoezi ya kukimbia sio mazuri .Kunywa maji ya kutosha na kula vyakula vyenye virutubisho na matunda kwa wingi,kumbuka kutumia net ya mbu malaria ni hatari.

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →