Mimba Miezi Mitano:Ukuaji Wa Mtoto Upoje,Mabadiliko Kwa Mama…

Mimba miezi mitano (wiki 20) unakuwa unashajua jinsia ya mtoto ,kama mama utakuwa ushafanya kipimo cha ultra sound.Mama anakuwa kafika nusu ya safari yake ya wiki 40.Mtoto anazidi kukuwa na mama kuelemewa na uzito wa mtoto kadri siku zinavyozidi kwenda.

Mimba miezi mitano

 

Mabadiliko ya mwili kwa mama

Mtoto anavyokuwa ndivyo mwili wa mama nao unatanuka ili kumtengenezea mtoto nafasi ya kutosha,mama kupata maumivu ya mwili kama maumivu ya tumbo chini ya kitovu, mgongo au kiuno n.k.

  • Mama anapata ndoto juu ya mtoto na ulezi kiujumla (motherhood)usijali ni kawaida ila kama ni ndoto za mbaya unaweza kusali na kukemea.
  • Kiungulia -mama anasumbuliwa sana na kiungulio kutokana mtoto kuanza kuota nywele kipindi hiki cha (wiki 20) ,na mabadiliko ya hormones mwilini  huchangia kuapata kiungulio pia.
  • Ngozi ya tumbo inatanuka na kukaza na kumsababishia mama  kuwashwa sana ,unachotakiwa kupaka mafuta mara kwa mara ili kukupunguzia hatari ya kupata michirizi (strech marks) na ngozi kuwa kavu tumia mafuta ya nazi ,cocoa butter lotion au palmer.
  •  Kutokwa vidamu au  maji maji ukeni (vaginal discharge)
  • Fizi(gums) za meno kutoa damu (ukiwa unapiga mswaki)
  • Kujaa kwa maziwa (kuongezea size)

 

 

Mabadiliko kwa mtoto

  • Kuanza kuota nywele kidogo
  • Muscles za mtoto zimeshaanza kukaza na sasa anaweza kujizungusha  na hapo kutamfanya mama ananze kusikia mtoto akicheza tumboni.
  • Anakuwa na urefu wa inches 10
  • Ngozi  ya mwili inajitengeneza na kutengenezewa white oily inayojulikana kwa jina la vernix caseosa itayompa kinga ya kumwepusha na  infection.

 

Ushauri  wa afyaborakwamtoto

Mama anatakiwa kula vyakula vyenye lishe bora,kunywa maji mengi ,kujipa mda wa kupumzika .Mazoezi ni muhimu yatakufanya usiwe na mwili wenye uchovu , kutosikia maumivu ya mgongo na sehemu nyingine za viungo , mazoezi yatakufanya ujifungue kwa haraka na urahisi.

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →