Mimba Miezi Minne Inakuwaje,Mabadiliko Anayosikia Mama

 

Mimba ya miezi 4(wiki 17)mtoto anakuwa na kuonekana umbo halisi la binadamu ,anakuwa na urefu wa 11cm na uzito wa 140g.

Hapo mama ndio anapoanza kupata uafadhali baada ya kutema mate sana ,kutapika,uvivu au kuumwa umwa asubuhi(morning sickness)

Mtoto ataanza kucheza (kupiga piga) tumboni  kwa mbali !

Hatari ya kuaribika kwa mimba inapungua mimba ikiwa miezi 4.

 

Ukuaji wa mtoto

 • Nywele -mtoto ataanza kuota nywele
 • kukua cells za ngozi .
 • Huanza kusikia( mama mjamzito anaweza ongea na mwanae)
 • kuoneka jinsia yake kama( msichana au mvulana)kwa kuchukua kipimo cha ultra sound.
 • Mapafu kuanza kujijenga.
 • Mifupa na misuli huanza kukomaa na ndio mana anaweza kucheza!

 

Mabadiliko ya mwili kwa mama –

 • Kupata  hamu kubwa ya kula!
 • Kupata kiungulia
 • Kutokwa Maji maji(ute)mweupe ukeni yenye ki harufu ni kawaida wanawake wengine hujikuta kubadili chupi kila Mara au kuvaa pad!
 • Kuongezeka uzito tumboni sababu ya kukua kwa mtoto!
 • Tumbo litaanza kuchomoza(kuonekana)

 

Ushauri toka afya bora kwa mtoto

Usitumie  pombe, sigara,bangi au madawa ya kulevya !Kula chakula chenye virutubisho, matunda,mboga za majani, kunywa maji kwa wingi na jipe mda wa kupumzika.

Tag rafiki

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →