Matumizi Ya Diaper /Nepi ,Mtoto Anatakiwa Kubadili Nepi Kila Baada Ya Masaa 2

Diaper na  nepi(prefold cloth diaper) ni mavazi mazuri kwa mtoto ila yanaweza kuwa sio salama iwapo mtoto ataachwa nayo kwa mda mrefu bila kubadilishwa.Matumizi ya nepi yamepungua  kwa sasa wengi wanatumia diapers , ni rahisi kutumika zinatoa usumbufu wa kufua mara kwa mara,sio rahisi kuchafua nguo za mtoto iwapo akijisaidia.

image

Kwa upande mwingine ni gharama sana , zinaweza leta allergy kwa baadhi ya watoto  sababu wanatumia chemicals kwenye kutengenezea diapers.Chemicals zinakuja kureact kwenye mwili wa mtoto na kumsababishia mzingo(allergy kwenye ngozi kupata vipele) japo kuwa kuna baadhi ya vyakula pia huleta allergy kwa mtoto.

 

 

Kwa matumizi ya  nepi(prefold cloth diaper) ni nzuri bei zake ni rahisi na ni salama zaidi kwa mtoto, kwa upande wa usafi zinatakiwa kulowekwa na kuzifua vizuri kisha zinyooshwe kwa pasi baada ya kukauka ili kuuwa vijidudu.Usitumie pini ya chuma kwenye kumfungianepi  mtoto ni hatari ikifunguka inaweza mchoma tumia ya plastic ni salama zaidi.

 

image

Mtoto anapojaza diaper kwa haraka iyo ni dalili tosha kwamba mtoto anakula vizuri na kushiba, kama mtoto diaper au nepi yake  amekaa nayo kwa mda mrefu bila kujaa (kavu) nidalili hali na kushiba vizuri au anaupungufu wa maji  mwilini.

 image

Aina ipi ya diaper ni nzuri?

Kuna brands tofauti za diaper hapa Tanzania kila moja inaubora wake na bei yake, ila kwa utafiti nilioufanya kwa mama tofauti, wengi waliniambia wanapendelea kutumia diaper za Huggies wakisema inamaterial nzuri na mtoto anaweza kaa nayo kwa mda bila kujaa kwa haraka.

unaponunua diaper za mtoto angalia yenye material ya cotton kwa ndani sio yenye plastic iyo ni hatari sana haziwezi pitisha hewa  na nirahisi mtoto kupata U.T.I, mfano mtoto amepata hajakubwa na kaveshwa diaper yenye material ya plastic kwa ndani haipitishi hewa ni mateso makali kwa mtoto na hili joto letu Tanzania.

Mtoto anahitaji kubadilishwa diaper / nepi kila baada ya mda gani?

Mtoto anahitaji kubadilishwa diaper au nepi kila baada ya masaa 2-3 iwapo hajapata choo kikubwa ,kama amepata choo kikubwa haina haja ya kusubiri mpaka yafike hayo masaa unatakiwa umbadili haraka .

diapers zinauzwa kwa size za ( namba) nakuzingatia umri na uzito wa mtoto, mfano watoto wachanga wanavaaga namba 1 , zingatia mtoto avae diaper inayoendana na uzito na umri usinunue diaper ya kumbana itamfanya kuto kuwa Comfort na kukosa kupata hewa.

 

Madhara ya diaper au nepi kwa mtoto akiachwa nayo mda mrefu

  • Unapomwacha mtoto na nepi au diaper kwa mda mrefu anaweza pata asthma .

  • Mtoto anahatari ya kupata UTI

  • kuunguzwa na kinyesi au mkojo

  • Kupata vijipele vidogo vidogo na kumwasha(diaper rash)

 

image

 

 

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →