Mafunzo Ya Kutumia Poti Kwa Mtoto(Potty Training)

Mtoto anavyozidi kukua  mama anapata maswali mengi ya malezi ,kama hili la kumfunza mtoto kutumia potty.Mzazi anajiuliza umri gani ni sahihi kuanza mfunza mtoto, wengi wanaanza funza mtoto akiwa na miezi (miezi 6-18) ila zoezi haliwezi kuwa rahisi sababu mtoto alie chini ya miezi 12 ni ngumu sana kujibana asijisaidie kwenye nepi au chupi sababu kibofu cha mkojo bado hakija komaa na kuhimili kukaa na haja kwa mda mrefu na hata iyo kumbukumbu hana ya kukimbia au kuomba kukaa kwenye potty.

 

image
L

Wataalamu wana sema umri sahihi ni kati ya miaka 2-3 hapo japo watoto wa kike wanawahi kuzoea kutumia potty kuliko wa kiume,mtoto anaweza kuongea au kukuonyesha ishara kwamba nataka kujisaidia kwa

  • Kuvua nguo zake

  • Kujibana sehemu za siri

  • Kukimbilia chooni

Kwa wale waishio nchi za  baridi inabidi wawe makini sana,sababu mtoto atajikojelea mara kwa mara  nguo zitakuwa mbichi kwa kila mda ,sio vizuri kipindi cha baridi kutampa maradhi na hata daycare hatokuwa comfort.Muda mzuri wa potty training ni summer time.

image

Dalili ya mtoto alietayari kufunzwa potty

  • Diaper yake kutokujaa kwa haraka yani masaa 2-3 bado inakuwa bado kavu.

  • Akikojoa au kupata hajakubwa anataka diaper ibadilishwe

  • Kukuonyesha choo na badaa ya kukuonyesha anajisaidia kweli

 

Hapo mzazi unapaswa kuanza mfunza mtoto kwa maneno kama kukojoa ni shishi au kupata haya kubwa na poo ,ili ajue utofauti wake utamfunza kunawa mikono kila baada ya kwenda chooni ili azowee tangu akiwa mdogo.Utamfunza kwenda kukojoa kila baada ya dakika 15 wakati wa mchana weka potty sehemu ya wazi  na akisikia kujisaidia anakwenda au atakuonyesha kwa ishara .Asubuhi akiamka mkalishe kwenye potty itaenda atazowea akiamka cha kwanza ni kukaa kwenye potty.

image

Mwepushe kuvaa nguo za kumbana zita mshinda  kujivua wakati wa kujisaidia ,watoto wengine wanakuwa wanalia hawataki kukaa itabidi umdanganya na toys au kitabu cha michoro au hadidhi utamwona anakaa na kusoma au kuchezea bila kusumbua ,kwa wale wenye vyoo vya ndani vya kukalia mnaweza nunua potty toilet seat ya kumwekea juu na akakalia wanauza na stol zake za kupandia mana bado ni mfupi kufikia.( kwenye super markets zinapatikana kwa bei ya kawaida tu) hiyo atatumia mpaka atakapo fika miaka 6-7

 

 

image
POTTY TOILET SEAT NA STOL YAKE KWA MATUMIZI YA NYUMBA ZENYE VYOO VYA KUKALIA

Usiku

Mida ya jioni utampunguzia kiasi cha kunywa vimiminika (juice,soda au Maji) kwa wingi  na anapaswa akojoe kabla hajalala na usiku akiwa amelala utamwamsha akakojoe tena Ili asije Kojoa kitandani na unaweza nunua ile mipia ya kutandika kindani kuzuia mkojo usifike Kwenye godoro.

 

Usafi

mzazi unatakiwa kuwa makini Nswala la usafi wa mazingira YA CHOO Na potty ya mtoto,osha potty Yake kila amalizapo Kutumia kwa ️Maji safi na weka ikauke juani kuua vijidudu ,potty au mazingira YA choo yakiwa machafu mtoto anahatari ya kupata infection.

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →