Madhara Ya Kuwachapa Watoto

Katika familia zetu tunazoishi tangu zamani tumekua tukitumia adhabu ya kuchapa watoto kama njia ya kuwakanya na kuwafundisha njia bora na tabia nzuri. Yaani imekua ni kawaida kabisa kumchapa mtoto kila akifanya kosa unachukua fimbo na kumpiga, ila sasa wataalamu wa saikolojia wanasema hii tabia ya kuwachapa watoto itawaathiri baade wakiwa wakubwa.

Madhara ya Uchapaji Watoto

Ukimchapa mtoto kunaathiri tabia yake ukubwani,Utafiti unaonesha kuwa adhabu ya kumchapa mtoto ina madhara. Watoto wanaochapwa mara nyingi huenda  watakuwa na tabia za kuchapa wengine mbeleni katika maisha yao na inahusihwa pia na ukatili kwa wengine.

Tabia mbaya na ya kuchapa wengine

Tafiti zinaonesha kuwa watoto wanaochapwa utotoni huwa wanajenga tabia ya kuwa makatili na wachapaji wakiwa wakubwa na watu wazima, na bahati mbaya hii inaweza kutokea kwa mtoto yoyote tu na kama wewe kama mzazi unampiga mtoto wako kila mara basi hali hii inaweza kumtokea mtoto wako.  Majambazi na wauwaji wengi wamegundulika kuwa walikuwa mojawapo ya watoto walionyanyaswa au kufanyiwa ukatili wakiwa wadogo. Kama tunavyojua wote tabia za watoto huwa zinajengwa kwa kiasi kikubwa  kwa kuiga wazazi au wakubwa wao wanachofanya hasa wakiwa katika umri mdogo.

Watoto Wanakosa Upendo na Kuwa na Kinyongo cha Kulipiza Kisasi

Nahisi hii unaweza kuikumbuka wakati ulipokua ukichapwa na mama au na baba. Yaani kuna wakati unatamani utakuja kumrudishia.  Mtoto anapochapwa hujenga hasira,kukata tamaa na hisia za kisasi na kukosa upendo.

Watoto wengi wanapochapwa huhisi wameonewa na humchukia aliyewaadhibu hata kama ni mzazi wake. Kwa hiyo adhabu za aina hii zikiwa zinatolewa kwa muda mrefu huweza kuwajenga watoto wasio na upendo kwa wengine na hata wao wenyewe, na hii unaweza kuiona kwa hali ya kaaida mtoto tangu anaanza darasa la kwanza anachapwa mpaka anafika darasa la saba kwa hiyo hii inakua ana madhara makubwa. Kuna kesi nyingi mashuleni wanafunzi wanawapiga walimu wao siku ya graduation yao, hii yote ni kwa sababu ya kuchapwa na hao walimu tangu walivyokua madarasa ya chini mpaka wanamaliza.

Kitu kingine ambacho unatakiwa kukikumbuka ni kwamba hasira za utotoni zinafukiwa ndani na zinakuja kulipuka wakiwa wakubwa,usishangae kwanini watoto wako wamekuwa na tabia za ajabu wakati uliwafundisha maadili mzuri.

 

Fimbo Zinamfanya Mtoto Apunguze Upendo Kwa Wazazi Wake au Walimu

Kwa hali ya kawaida  tu yaani watoto wenyewe wakiadhibiwa kwa kuchapwa fimbo wenyewe wanaona kama wanaonewa, auadh kuna baadhi ya makosa ambayo mtoto anaweza kufanya alafu yeye mwenyewe akajiambia kwa hilo kosa hawezi kuchapwa ataishia kugombezwa tuu, sasa akirudi nyumbani mzazi anampiga, kwa hiyo kwa kitendo hicho mtoto atamchukia mzazi wake kwa kuwa kampiga kisa kafanya kosa dogo. Kwa hiyo adhabu ya fimbo hupunguza upendo wa wazazi  na walezi.

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →