Mabadiliko ya Mwili Baada Ya Kujifungua.

Kama ulikua hujui basi taarifa ni kwamba mama mjamzito akishajifungua huwa kuna baadhi ya mabadiliko mwilini ambayo huwa yanatokea. Kuna ambayo huwa ni mazuri na mengine, unaweza usiyapende. So nimekuwekea list ya baadhi ya mabadiliko ambayo kama yakikutokea usishangae.

Utapoteza Kilo Ngapi?

Ukijifungua una uwezekano wa kupoteza Jumla ya Kilo 12. Utapoteza kilo 7 au 8 kwa sababu ya mtoto ametoka tumboni na kuna kilo zingingine kama kutokwa na damu na mambo mengine ya mwilini baada ya mtoto kutoka tumboni ila karibia kilo 12 kuna uwezekano wa kuzipoteza.

Mwili wako hautarudi katika hali ya kawaida kama ulivyokua kabla hujapata ujauzito na vile vile mwili wako utaendelea kupungua uzito wakati wa recovery kwa sababu mwili wako utaendelea kutoa yale maji ya ziada ambayo yalikua mwilini kwa ajili ya mtoto wa kati wa ujauzito na kemikali zingine zilizokuwa kwenye damu, kwa hiyo tegemea hili kutokea,. Mara nyingine hii sio lazima kwa kila mwanamke ila huwa inaweza kukutokea kwa hiyo kama ikikutokea wala usishangae kwa sababu ni kawaida kutokea hivyo.

Baada ya kujifungua zile siku za mwanzo utakua unapata na haja ndogo ya kila mara na baada ya wiki ya kwanza  utajikuta umepunguza uzito wa kilo 1 kwa sababu ya maji unayoyatoa mwilini kwa njia ya haja ndogo, na hii inategemea kutokana na kiasi cha maji ambayo ulikua unakunywa kipindi cha ujauzito, kama ulikua anamjali sana mtoto wako na ukawa unakunywa maji ya kutosha basi hayo maji baadae utayapunguza na kama ulikua unakunywa kidogo basi haitachukua mda kuja kuyapunguza.

Kuonekana Kama Mjamzito.

Kuna baadhi ya wanawake baada ya kujifungua mtoto unaona tumbo lake bado linaonekana kama vile ana ujauzito. Hii huwa ni kawaida kwa sababu mishipa ya tumbo huwa inapanuka kwa sababu ya ujauzito ni hivyo huwa inachukua mda kuja kujirudi na kuwa katika hali ya kawaida, Mara nyingi hii hali inaweza kwenda kwa wiki moja au mbili na wanawake wengine wanaweza kwenda hata mwezi, kwa hiyo hii hali ikikutokea ndugu yangu wala usishangae ni kawaida.

Utegemee nini Kama Utakuwa unanyonyesha.

Mara yako ya kwanza Kumyonyesha mtoto mara nyingi matiti unaweza kukuta ni magumu kidogo na baada ya kuanza kutoka yatarudi na kuwa kawaida na rahisi kwa mtoto wako kunyonya, na mara nyingine unaweza kuyaona kama mazito na sometimes utaona kama yanakusumbua ila baada ya siku mbili tatu yatakuwa sawa kwa sababu mtoto atakua ananyonya kwa hiyo yatapungua.

Kumyonyesha mtoto wako kila  mara ni kitu cha muhimu sana na ni njia nzuri ya kutengeneza mahusiano mazuri na mtoto wako tangu akiwa mdogo.

Itakuaje kama hutotaka kunyonyesha mtoto wako?

Ukushajifungua mwili wako utaanza kutengeneza maziwa na matiti yako yataanza kuwa mazito na kuna maumivu kidogoo kwa mbali utakuwa unayasikia ila baada ya muda siku chache yataisha kwa sababu hapa huwa sometimes inamfanya mama asiwe na amani kidogo. Haya maumivu yanaweza kukaa kwa siku tatu au siku tano.

Wakati wote vaa sindiria ambayo inaweza kuyabeba maziwa vizuri na vile vile isiyabane sana matiti.

 

Kuhusu Nywele.

Kama nywele zako zilikua zimeanza kupunguza kasi ya kukua na kuwa ndogo ndogo, basi baada ya kujifungua kuna uwezekano wa nywele zako kupotea na kupungua kinchwani. Hii huwa inatokea kwa baadhi ya akina mama hasa wale wanaojifungua kwa mara ya kwanza. Usijari hazitatoka zote mpaka uwe na kipara, ila zitapungua tuu.

Wakati una ujauzito kuna homini ambazo huwa zinasababisha nywele kupungua na kupunguza speed ya ukuajii wa nywele kwa mda, baada ya kujifungua ndio zinaweza kuongeza speed ya kupungua kabisaa, na baada ya hapo kama baada ya miezi mitatu au mitano nywele zitaanza kurudi katika hali yake ya kawaida na kuendelea kukua kawaida. Kwa hiyo kwa maneno mengine kama una ujauzito na ukagundua kuwa nywele zako zinapungua basi kuna uwezekano hizo nywele zitaendelea kupungua baada ya kujifungua tena alafu baada ya miezi mitatu mpaka mitano ndio zitaana tena kuota kama kawaida. Hii sio kwa kila mwanamke so we jiangalie  tu  kama ukiona nywele zinapungua usishituke sana ni hali ya kawaida tu.

Kuhusu Ngozi Yako.

Kutokana na maswala ya mtoto na kubeba ujauzito, kuulea na ukijumlisha mambo ya kazi za hapa na pale na stress na ile hali ya kuingia katika hali ya kulea mtoto huwa kunaleta mabadiliko makubwa kwenye mwili wako. Kuna wakati wanawake wengine wanaweza kuwa na ngozi nzuri wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua ngozi hubadilika.

Kama kuna mistari huwa inatokea baada ya kujifungua (streach marks) na mara nyingine huwa kuna misitari katikati ya tumbo , hii misitari huwa inapotea baada ya mda japokuwa streach marks mara nyingine zinaweza zisipotee kabisa ila zitapungua tuu kwa mbali.

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →