Maandalizi Ya Mama Mjamzito Kwa Ajili Ya Mtoto

Maandalizi ya mama mjamzito kwa ajili ya mtoto ni muhimu kabla hajajifungua.Mama anaweza kuanza fanya shopping baada ya kufanyiwa Ultra sound kujua jinsi ya mtoto ,ili kuepuka gharama ya kununu nguo mara mbili iwapo unakosea jinsi ya mtoto.

 

image

Mimba ifikapo miezi 6-7 hapo mama anaweza anza kununua mahitaji ya mtoto utaandika list yako kam hii

 • Nguo-ukinunua nguo za mtoto usinunue size ndogo sana ,sababu watoto wachanga wanakuwa haraka mno.

 • Kofia-mnunulie 2-3 ni muhimu mtoto mchanga kufunikwa kichwa.

 • Masweta-nunua 2 yatamsaidia jioni kuwakuwa na kabaridi.

 • Taulo-1.

 • Soksi-nunua pair 3 au zaidi.

 • Beseni la kuogea-1

 • Sabuni au shampoo ya mtoto isio na harufu kali.

 • Sanduku au kabati la kuhifadhia nguo zake.

 • Nepi au diapers-utanunua nepi pair 12 au zaidi ukiweza ,ili iwe rahisi mtoto kubadilishwa nepi mda wowote iwapo zimechafuka.

 • Neti kuepuka mmbu-Malaria ni hatari kwa watoto usimlaze bila kutumia neti.

 • Bibs-kama kaapron ivi utamfungia shingoni akicheuwa au udenda ukimtoka hautomlewesha.

 • Cotton buds-kusafishia masikio .

 • Mafuta ya nazi -watoto wachanga wanakuwa na ngozi kavu ,mafuta ya nazi yanawafaa zaidi.

 • Wipes au vitaulo vidogo -utatumia kumfutia akjisaidia au kumfutia baada ya kumnawisha na maji safi.

 • Kitana.

 • Nail care-utatumia kumkatia kucha ili mtoto asijikwangue usoni.

 • Khanga au vitenge-mama atatumia kumbebea au kumfunika.

 • Kitanda cha mtoto kwa watakao weza afford-kina mfanya alale kwa usalama zaidi tofauti na kitanda cha watu wazima ni rahisi kuanguka akijigeuza.

 • Mashuka 2-3 ya kutandani na kumfunikia.

 • Kiti chake cha kumkalisha kwenye gari- kwa wenye magari epuka beba mtoto bila kiti chake na kumfunga mikanda itamwepusha  kurushwa nje ya gari au kujigonga vibaya iwapo itatokea ajali.

 • Stroller-ni kigari anachokaa na kusukumwa mtoto ila iwapo mzazi utapenda ndio utanunua,na ukimkalisha hakikisha umemfunga mikanda ili asianguke.

 

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →