Lini Unaweza kurudi Kazini Baada ya Kujifungua

 

Kwa kawaida kuanzia week sita baada ya kujifungua ndio mda ambao huwa ni kawaida unaweza kurudi kazini. Kuna baadhi ya wanawake wanaweza kujisikia kuwa wanahitaji kurudi kazini mapema sana baada ya kujifungua na hii inategemea na uhitaji wa kazi zilizopo na uwezo wa watu wa kumsaidia nyumbani. Kama nyumbani una watu wa kukusaidia basi unaweza kurudi kazini mapema. Wakati unapanga likizo ya kujifungua hasa kama ni mtoto wako wa kwanza usidhanie kuwa itakua rahisi tu na unaweza kurudi kazini mara moja, yaani kuna wa kati utajikuta huwezi kufanya kazi  huku unamhudumia mtoto.

 

Sasa wakati unajaribu kujuliza ni mda gani unaweza kurudi kazini baada ya kujfungua basi ehm jiulize haya maswaali kwanza….

Unafanya kazi kwa masaa mangapi kwa siku? Kama unafanya kazi masaa 20 kwa week na ukarudi kazini kabla ya week sita basi utakua unajiletea balaa na  hatari kwenye mwili wako. Unahitaji kupumzika na kupona kwanza kabla hujarudi kazini.

 

Je Kazi yako inahitaji nguvu?

Kama kazi yako huwa inahitaji nguvu au kubeba vitu vigumu basi kwa kweli inabidi utulie tu mpaka week sita zipite ndio urudi kazini. Vile vile kama unatumia nguvu sana kazini, na ukirudi nyumbani unaweza kukosa nguvu hata za kumbeba mtoto anyonye na pia kabla ya week sita yaani hata mwili wenyewe unakua hauko tayari kwa aina hizo za kazi kwa hiyo unaweza kuwa unajiumiza mwenyewe.

Unaweza kupata mda wa kupumzika kama ukihitaji?

Wanawake wengi huwa wanahisi wanahitaji kupumzika mida ya mchana. Kama uko nyumbani unaweza kufanya kazi zako hapo wee af mda wowote tu unaweza kuamua mwenyewe kupumzika hata masaa kumi. Sasa huko ofisini kuna sehemu utapata angalau mda wa kupumzika na boss akakuelewa!? Kama unajua kabisa ofisini hawatakuelewa wakikuona unalala basi mama wewe tulia tu mpaka week sita ziishe na pale utakapoona mwili unaruhusu kurudi kazini, we rudi tu ukaendelee na kazi.

Kama unanyonyesha je kuna sehemu unaweza kukaa na kunyonyesha mtoto.

Yaani ni lazima kuweka hii mipango mapema kabla kwa sababu unaweza kujikuta unashindwa kumyonyesha mtoto wako wakati anapokuhitaji na kuleta matatizo kwa wafanya kazi wenzio kwa hiyo kama unaona haiwezekani basi wewe tulia tu mpaka utakapo pona ndio urudi kwa nguvu ya hatari.

 

 

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →