Kuvimba Kwa Matiti(Maziwa):Baada Ya Mama Kuacha Kunyonyesha

Zoezi la mama kumwachisha mtoto kunyonya  linakuwaga gumu kidogo kutokana na changamoto za mtoto na mwili wa mama kupata maumivu. Mtoto anatakiwa anyonyeshwe mpaka afikishapo miaka 2,ila iwapo mama anajisikia  kuendelea mnyonyesha mtoto anaweza endelea haina tatizo .Maziwa ya mama huwa yanavimba na kuleta maumivu makali iwapo anasitisha kumnyonyesha mtoto.

 

 

 image

 

 

Kuna umuhimu wa mama kujiandaa  kabla hajamwachicha mtoto kunyonya kwa

 • Kupunguza kiasi na masaa ya kunyonyesha  kwa siku ,itamsaidia mtoto kuzoea taratibu kabla kuachishwa kwa mara moja.Mfano  asubuhi anyonye mara 1 -mchana  mara 1, usiku mara 1, utampunguzia tena baada ya kuzoea hii ratiba na kuanza mnyonyesha asubuhi 1 na usiku 1 siku zinavyoenda  hatonyonya asubuhi ,atabaki kunyonya usiku tu,usiku nayo utakuja mwachisha kabsa,utampa maziwa au uji kabla hajalala hapo atakuwa kesha sahau nyonyo na huta zalisha maziwa kwa wingi yatakauka.

 

 • Kumzoesha mtoto kutumia chupa ya kunyonya kwa kumwekea  itamfanya kuhisi kama ananyonya ziwa  la mama

 • Mama aache kupump maziwa- atakavyo pump ndio yanavyozidi kuzalishwa.

 

 

Njia zipi zitamsaidia mama kuachisha kumnyonya mtoto

 

 

 • Mama alale chumba tofauti na mtoto / mtoto anaweza pelekwa kwa bibi au ndugu kwa kipindi cha siku 5-7 hapo itamsaidia mtoto kuacha kunyonya kwa haraka sababu hato pata mda wa kumwona mama yake.

 • Kuto kuvaa au kuvua nguo mbele ya mtoto akiona matiti atakumbuka kunyonya

 • Kuweka plasta kawenye titi na kumtishia ni mdudu ataogopa na kuacha

 • Michezo-akikumbuka kunyonya mdang’anye kwa michezo kuchezea vitu vya kuchezea(toys)

 • Epuka kumbeba beba mara kwa mara (cuddle)

 

 

 

Njia ya kupunguza maumivu ya matiti baada ya kuacha kunyonyesha

 

Kuachishwa kwa mtoto kunyonyeshwa au mtoto kutonyonyeshwa kwa mda mrefu kuna mwadhiri mama na kumpa maumivu sababu maziwa yanaendelea kunazalishwa kama kawaida na kujaa kwenye titi bila kunyonywa hii hali inaitwa engorgement,inamfanya mama awe discomfort hivyo kunanjia za kupunguza maumivu kwa kutumia

 • Maji -tumia maji vugu vugu kwa kuoga jimwagie kwenye titi  au weka maji vuguvugu kwenye taulo na kanda titi.

 • Cabbage leaves-chukua kabichi (majani) bila kukatwa katwa weka kwenye matiti valia ndani ya brazia kwa dakika 30 kwa kila ziwa fanya mara 3 kwa siku,inapunguza kuzalishwa kwa maziwa na kukusaidia kujisikia vizuri.

 

image

 •  Brazia -vaa brazia ya kulegea

 • Antibiotic-mama kama amezidiwa na maumivu makali ,titi kuvimba na kupata homa hii inaitwa (mastitis) titi linakuwa na infection anaweza kutumia antibiotic huwa inatokea kipindi hiki cha kumwachicha mtoto kunyonya.

 • Mint leaves-tumia majani ya mint ,chemsha maji weka minti epua chuja na kunywa  maji inapunguza kiasi cha uzalishwaji wa maziwa (majani ya minti yapo masokoni kama kariakoo,kisutu n.k kwa bei rahisi )

 • Barafu-weka barafu kwenye kitambaa then jikandie itasaidia

 • Pain killer-tumia dawa ya kupunguza maumivu

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →