Kupitiliza Mda Za Kujifungua Kwa Mama Mjamzito (Overdue Pregnancy)

Mama mjamzito anapopitiliza siku za kujifungua kwenye wiki ya 40 ,anakosa amani na kujiuliza maswali mengi. Mimba ikifika wiki 41-42 hapo inakuwa imepitiliza muda  (overdue).

Kuna sababu tofauti zinazo sababisha mama kupitiliza siku zake za kujifungua.

 

 

Baadhi ya sababu za kupitiliza kujifungua ‘overdue’:

–  Iwapo mama atahesabu siku zake vibaya basi hapo ataona amepitiza siku za kujifungua

– Kama ulishazaa kwa mara ya kwanza na ukapitiliza

basi uzao wako unaofuata  tatizo linaweza kujirudia.

– Kupitiliza kujifungua pia hurithiwa kutoka kwa  familia.

– Watoto wa kiume mara nyingi  huchelewa kutoka tofauti na wa kike.

– Matatizo ya kondo la uzazi kushindwa fanya kazi ipasavyo.

Mama anapopitiliza kujifungua anakuwa anakosa raha, mwili huchoka,anashindwa kulala ,anapata kiungulia na kukosa choo.

 

MADHARA YANAYO JITOKEZA MAMA ANAPOPITILIZA SIKU ZA KUJIFUNGUA

Mimba inapokuwa zaidi ya wiki 41, afya ya mtoto inakuwa hatarini kama ifuatavyo:

– Mtoto anaweza kupata choo (kujisaidia) na kula kinyesi akiwa tumboni.

– Kupungua kwa kiwango cha maji yanayomzunguka mtoto (ambiotic fluid).

– Mapigo ya moyo ya mtoto kupungua.

– Mama anaweza  kuzaa kwa c-section sababu mtoto kesha kuwa mkubwa.

 

MAMA ANATAKIWA KUFANYA NINI?

Mama anapopitiliza kujifungua anahitaji kuwa karibu na daktari mara kwa mara. Iwapo utapata dalili yoyote usiyoielewa, wahi hospitali, inaweza kuwa kifafa cha uzazi au tatizo lolote kubwa.

 

Mimba inapokuwa wiki ya 42 -43 ni  vizuri daktari apime mapigo ya moyo ya mtoto,kuangalia kucheza kwa mtoto na kiasi cha maji maji yaliopo(amniotic fluid). Sababu yanapo pungua husababisha mtoto kunyongwa na kondo la nyuma (umbilical cord) shingoni.

Mimba haitakiwi  kukaa kwa muda mrefu, iwapo  mama hatapata uchungu, daktari atamwanzishia uchungu ili njia ifunguke na iwapo itashindikana basi atafanyiwa upasuaji.

 

ANGALIZO:

Kuna baadhi ya wanawake  njia zao za uzazi haziwezi tanuka, wana maumbile madogo sana, hata wakianzishiwa uchungu kwa muda mrefu bado lazima watazaa kwa upasuaji .Ni vizuri ukazalishwa na daktari aliyekuzalisha mwanzo, kwa sababu anajua historia yako ya uzazi iwapo ni uzazi wako wa pili au zaidi.

 

 

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →