Juice Ya Karoti Na Machungwa Kwa Watoto Kuanzia Miezi 7

Juice ni muhimu kwa watoto zinawapa vitamins mwilini, nivizuri ukampa zile fresh ambazo unatengeneza mwenye nyumbani bila kuwekwa chemicals,juice za madukani anaweza kunywa ila isiwe mara kwa mara.

 

 

image

Mahitaji

  • Karoti 2-3

  • Machungwa 2

 

Jinsi ya kuandaa

Osha machungwa na karoti kwa maji safi kisha ,kwangua karoti kutoa maganda,chukua kifaa cha kukwangulia karoti kwangulia ule upande wenye vitundu vidogo .image

 

Kamua upate yale maji ya kaaroti ,chuja na chujio weka pembeni,kata chungwa na kukamua juice yake ,chuja na changanya na ile juice ya karoti,koroga usiweke sukari.Unaweza mpa mtoto kuanzia miezi 7na kuendelea.

 

NOTE.Kwa matumizi ya mtu mzima unaweza weka kwenye friji ikapata ubaridi ndio ukanywa.

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →