Jinsi Ya Kulea Watoto wa Ki- Digital

Kulea mtoto wa kidigital

Kama ulikua huna habari basi naomba nikwambie kuwa kuna watoto wa kidigital. Yaani hawa watoto wana mambo, kwanza wanataka kujua kila kitu kabla ya umri wao, wanauliza maswali ambayo yaani unabaki kujiuliza alikua anafikiria nini, ni watundu kuliko sie tulivyokuwa wadogo, yaani hawatulii kabisa, shuleni basi ukimpeleka siku zingine hataki kwenda kwa visababu vya ajabu ajabu tu ambavyo hata sio vya msingi, mfano mtoto jana kaenda kulala vizuri tu wala hana hata ugonjwa wowote asubuhi unaenda kumuamsha aende shule anakwambia tumbo linauma, mara kichwa kinauma, mara sijui soksi sizioni yaaani sababu nyingi. Hao ndio watoto wa kidigital, na hapo bado maswala ya utandawazi mitandao ya kijamii, TV internet na hivyo navyo ndio wanavijua tangu wadogo.

Tabia ya mtu inatokana na malezi aliyoyapata kwa kiasi kikubwa toka kwa wazazi,pia toka kwa walimu mashuleni, mafundisho ya dini,na toka kwa watu anaoonana nao na kuchangamana nao kila siku za maisha yake hasa wakati wa umri mdogo. Kulea watoto kulingana na tamaduni zetu katika karne hii ya teknolojia ni changamoto kubwa.

 

Watoto wa dijitali kwa kweli wanafahamu mambo mengi sana kuliko  wanavyotakiwa kufahamu katika umri husika jambo

ambalo linaleta balaa kwa wazazi wakati wa kuwalea hawa watoto na unakuta  wazazi wengi wa sasa ni wa zamani ambao walizaliwa kipindi ambapo teknolojia haikuwa katika kiwango hiki na mfumo wa malezi walioupata unatofautiana  na wa sasa na pengine haufanyi kazi katika mazingira ya kisasa kwa hiyo unakuta mzazi asipokuwa makini inakua ngumu kumlea kwa sababu unakuta mtoto anajua vitu vingi kuliko mzazi mwenyewe na hii

 

hali inapelekea hadi mtoto anaanza kumfundisha mzazi wake sasa!! Sasa hii hali ikiendelea hivi Mzazi anakosa kujiamini katika jukumu lake la kumfundisha mtoto kwa kuwa anatambua kuwa mtoto ni mjuaji wakati mwingine kumzidi,na mzazi mwenyewe  anaweza kuamua kutofanya jukumu lake la kumfundisha kwa kujua mtoto anafahamu tayari. Wakati mwingine inakuwa si sahihi. Kitu kingine mtoto tatambua baada ya muda kuwa mzazi wake hafahamu mambo mengi na kuwa yeye anafahamu zaidi. Hivyo naye anaacha kuuliza au kutaka kufahamu toka kwa wazazi. Hivyo anaweza akafanya vitu kwa ufahamu wake tu binafsi au kwa kutafuta msaada sehemu nyingine nje na wazazi wake.

Mtoto wa ki-digital

 

Wazazi na walezi wanaweza wakaweka udhibiti nyumbani kwa kufanya yafuatayo:

Kutoweka TV vyumbani kwa watoto, kuna baadhi ya wazazi jamani inabidi tukubali wanaupendo wa kupitiliza. Yaani anampenda mtoto wake hataki mtoto apate shida so anamtimizia mahitaji yote hadi mtoto akitaka TV chumbani anawekewa. Sasa hii hali sio nzuri maana huko wewe kama mzazi hujui mtoto anaangalia nini huko peke yake kwa hiyo wakati wewe unaona unamfurahisha mtoto wako kwa kumuwekea TV chumbani basi kumbuka kuwa kuna vitu vingi anajifunza ambavyo wewe huvijui na njia rahisi ni kutoa hiyo TV chumbani kwake.

Kuzui sinema zisizohitajika kwa watoto majumbani, hii ni kitu muhimu sana kwenye upande wa TV. Kuna story nyingi kwenye hizi TV jamani kama mnavyojua, kuna movies, series, documentaries, vipindi vya watoto, vipindi vya wanyama yaaani vipindi chungu nzima mpaka mtu unashindwa uangalie kipindi gani. Basi kama unalijua hilo basi mchagulie mtoto wako baadhi ya vipindi aangalie sio kila kipindi umuache aangalie.

 

Udhibiti wa Matumizi ya Simu:

Hizi simu sio nzuri kwa watoto hasa kama bado ni wadogo sana, Lakini kama si lazima mtoto awe na simu basi wazazi wasimpe simu huyo mtoto au kam ni kumpa basi wazifuatilie kujua nani anapiga na kupigiwa na ujumbe unaotumwa kwa kuzipitia simu moja kwa moja au kutumia programu maalumu katika simu zitakazo tuma ujumbe kwa mzazi au kwa kupata taarifa toka makampuni yanayotoa huduma za simu.

Udhibiti wa Intaneti na Mitandao ya Kijamii

Wazazi wanaweza wakatumia programu katika simu kufunga baadhi ya taarifa au tovuti zisizohitajika kwa watoto. Watoa huduma wa intaneti wanaweza wakafanya hivyo pia kufunga taarifa ambazo hazihitajiki katika simu ya mtoto.

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →