Hospital Labour Bag -Bag La Kwenda Kujifungulia Mama

Mama mjamzito anatakiwa kuandaa bag lake atakalo kwenda nalo  hospital kujifungulia pale muda unapokaribia wiki ya 36-40 .Unatakiwa kufanya maandalizi mapema sababu unaweza patwa na uchungu kabla ya siku za makadirio.Unatakiwa uplan hospital utakayo jifungulia kabla ya kujifungua inakuwa rahisi kwako na ni vizuri uchague ya karibu ila yenye huduma nzuri.

 

Hospital labour bag

 

List ya mahitaji yanakuwa ni yako na ya mtoto ,

 

1:Khanga au vitenge pair 2-3

2.Chupi za size kubwa sio za kukubana pair 4-5

3.Maternity pads zinauzwa pharmacy 5000TSHS

4:Breast pads /nursing pads (kuzia maziwa yasivuje)

5:Bras/brazia za kuvaa pair 2 za kunyonyeshea au za kawaida

6.Nguo zako za kubadili 2-3 kwa wale wanao penda madera au magauni mapana mapana yanafaa.

7.Slippers/ kandambili

8:Chanuo kama ukiwa ujasuka

9.Body lotion yako

10:Dawa ya mswaki na mswaki

11:Tochi kwa wale wanaishi maeno ya kukatika umeme

12:Taulo ndogo ndogo unaweza tumia wewe na mtoto pair 3

13.Simu yako na chaji

14:Camera au video camera kwa wale watakao jifungulia  wanaweza chukua kumbu kumbu yako.

15:Lip balm kupaka mdomo usikauke hata ukija tembelewa unaona aibu

16.Deodorant (kupaka makwapani) usafi bado muhimu

 

Hospital labour bag

Mahitaji ya mtoto

 

17:Nguo zake pair 5-10

18.Diaper /nepi pair

19:Mfuta yake

20:Kitana

21:Nail cutter(kukatia kucha)

22.Soksi pair 2-3

23.Kofia yake

24:Kiblanket chake kumfunikia akilala au akibebwa

25.Baby wipes

26.Sweta 1-2

 

kwa wale watakao jifungulia private hospitals kunaa baadhi ya vitu hutakiwi kwenda navyo ,ila kwa wale wanaojifungulia hospital za selikalini  wanatakiwa kubeba kama

 

1:Ndoo ya kuwekea nguo chafu

2:Pamba,viwembe,

3.Cloves

 

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →