PISHI LA BOGA NA MAZIWA(MASHED PUMPIN)

 

Huu ni mwendeleze wetu wa vyakula vya watoto kuanzia miezi 6 na kuendelea.Hapa utamwandalia boga.

 

Mahitaji

Nusu ya boga

Butter kijiko 1 cha chai

Maziwa 1/2 kikombe

 

Jinsi ya kuandaa

Menya boga lako ,katakata vipande vidogo osha na weka kwenye sufuria tayari kuchemsha na maji.Chemsha kwa dakika 15-20 mpaka lilaineke .Utachuja maji na kusaga unaweza saga na handmixer au blender.aina haja ya kuweka chumvi kama ni yamtoto chini ya mwaka 1.Utaweka maziwa na butter wakati wa kusaga hakikisha kinakuwa laini kabsa na tayari kumlisha mtoto.

Kwa mtoto aliejuu ya mwaka 1 unaweza mwekea na mchuzi wa nyama,samaki,kuku au mboga yoyote akala nayo. Huu mlo unavirutubisho vingi muhimu kwa mtoto.

 

NB

Epuka kupiga chakula kwa moto mkali sana na usipike kwa muda mrefu kupoteza virutubisho.