Folic Acid :Faida Zake Kwa Mama Mjamzito Na Mtoto

Folic acid ni mkusanyiko wa vitamins(B12,B9,C,folate n.k)unaotoka kwenye matunda na vyakula unaotengenezwa mfumo wa supplement(vidonge) vinavyosaidia mwili kuzalisha damu ya kutosha na kumpa kinga mama mjamzito ili aweze kuzaa mtoto asie na ulemavu.Folic acid inaweza kutumiwa hata na mtu wa kawaida kutibu mapungufu ya damu na kuepusha maradhi mengineo kama cancer ,matatizo ya moyo na ugonjwa wa kupooza.

 

image

Folic acid kusupport ukuaji wa mtoto na kumwepusha na tatizo  (Neural tube defect) .

 

       Mathara ya upungufu ya folic acid kwa mama mjazito

 

 •  Mama na mtoto  kukosa ya damu  ( anaemia)

 • Kuadhiriwa kwa ubongo  na uti wa mgongo wa mtoto

 • Mtoto kuzaliwa mgongo wazi  / kuzaliwa na uvimbe mkubwa mgongoni

 • Mtoto kutozaliwa na kichwa kikubwa kuzidi umri wake na kumwelemea,

 • Mtoto kuzaliwa mdomo juu ya lips (panakuwa hapafungi)

 • Mtoto kuzaliwa na kichwa chenye mapungufu kinakuwa na umbo kama la chura

 • Mimba kuharibika(Miscarriage)

 • Mtoto kuzaliwa njiti

 • Kuleta ulemavu wa miguu

image
WATOTO WALIOZALIWA NA MAPUNGUFU YA KICHWA KIKUBWA,MDOMO WAZI,MGONGO WAZI NA KICHWA UMBO LA CHURA

Hizi folic acid zipo za aina tofauti na zinatolewa kwenye vituo vya afya ,kama mama mjamzito anatumia kipindi cha miezi 3 ya mwanzo mwa mimba(first trimester) au kipindi mama anatafuta mimba anatumia ,kama mama mjamzito bado hajatumia unaweza ulizia klinik wakakupa ni muhimu ,mjamzito akitumia folic sio rahisi kupata tatizo la upungufu wa damu,kupunguza hatari ya kupata cancer na matatizo ya moyo.

 

image

 

 

Kiasi gani mama anatakiwa kutumia folic acid

 • Mama mwenye mimba anatakiwa atumie isipite kuanzia wiki 3-4 hapo mtoto ananza tengenezwa ubongo na spinal cord(uti wa mgongo) ,tumia kiwango cha 400micrograms

 • Mama anaetafuta mimba anatumia kiasi cha 400micrograms miezi 3 kabla

 • 5Mg kwa mama alieshawahi  kuzaa mtoto mwenye matatizo hayo,ni vizuri ukawahi kutumia mapema kuna uwezekano wa kuzaa mtoto mwenye hayo matatizo tena vizuri kunywa mapema ili umwepushe

 • Mama mwenye uzito mkubwa au diabetes nae ana hatari ya kuzaa mtoto mwenye mapungufu, vizuri wakatumia 50mg za folic acid

Vizuri ukaongea na daktari mapema juu ya vipimo vya folic na umwelezee afya yako na kama ulisha zaa watoto wenye matatizo ya kichwa kikubwa,mgongo wazi n.k atajua kukupa kiasi gani cha folic kama uongezewe kipimo.

 

 

Vyakula vyenye vyanzo vya folic acid

Mama anaweza kaputa folic acid kupitia vyakula na matunda kama

 • Machungwa au ndimu

 • Parachichi

 • Papai

 • Nyanya

 • Bamia

 • Viazi vitamu

 • Dagaa

 • Maharagwe meusi/ njegere

 • Mayai ya kuchemsha

 • Brown rice n brown bread

 • Pasta / tambi ndefu

 • Broccoli

 • Spinach

 • Maharage mabichi

 • Beetroot

 

Ushauri toka kwa afyaborakwamtoto

Mama anaenyonyesha nae anatakiwa kutumia folic acid sababu mtoto bado anahitaji folic mwilini kwa ukuaji wa ubongo na mengineo ataipata kupitia maziwa ,pia itakusaidia kuongeza damu uliopoteza kipindi cha kujifungua.Mjamzito zingatia kutumia dawa unazopewa klinik japo zinaladha mbaya na zinaweza badili rangi ya kinyesi ikawa nyeusi.

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →