Chakula Cha Mtoto Kuanzia Miezi sita

️️Watoto wanapofikisha ️Miezi sita ndipo wanapoanza kula chakula vigumu. Leo tutamwandalia mtoto chakula chepesi na kinasaidia kupata choo kwa urahisi!

Mchanganyiko wa boga,viazi na karoti baada YA kukatakata
Mchanganyiko wa boga,viazi na karoti baada YA kukatakata

Muda wa kupika dakika 30

MAHITAJI.

1.Boga 1/2
2.Viazi mviringo 2
3.karoti 1
4.Olive oil ️Au siagi isiyo na chumvi.
5.Maziwa au supu nyama ️Au kuku ️Au

JINSI YA KUPIKA

Menya boga ,viazi na karoti na safisha kwa Maji safi,kata vipande vidogo vidogo .

Bandika sufuria jikoni likipata moto weka olive oil ️Au butter,weka mchanganyiko Wako wa boga,viazi na karoti ongezea vikombe 2 funika wacha kiive kwa dakika 25.

Epua tayari kusaga kwenye blenda kama huna tumia kuponda ponda kwa uma.

‼️‼️Kwa ️watoto wa ️Miezi 6-7 usitumie mchuzi tumia Maji sababu ️️watoto wanaanza kula nyama wakiwa na ️Miezi 8.Utakapo saga ️unaweza ukaweka Maziwa ya mama ️Au kopo .

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →