Zawadi Zipi Anastahili Pongezwa Mama Alietoka Kujifungua Au Kupewa Kwenye Sherehe Ya Baby Shower

Inakuwa jambo la furaha sana pale mama anapofanikiwa kujifungua salama baada ya kubeba mimba kwa miezi tisa. Na kwa ndugu ,rafiki ama jirani huwa wanapata shida sana kufikiria zawadi gani tupeleke wakati wa sherehe za baby shower ama kwenda kumuona mzazi. Leo tuone zawadi muhimu ambazo zaidi ya kadi unaweza kuambatanisha pamoja na kumfanya mzazi afurahi pale anapopata zawadi yako za pongezi   ni kama ifuatavyo:

 image

 •   Toys za aina mbalimbali ambazo zitaongeza uwezo wa kufikiri kwa mtoto ama kumhamasisha awe na usikivu,chagua zenye rangi rangi za kumvutia hakikisha unaponunua uangalie umri toys zinaendana na umri wa mtoto.

 

image

 

 • Vifaa mbalimbali vya kitandani kwa mtoto kama mto wa kulalia,mashuka yenye picha mbalimbali, blanket kwa wale wanaoishi mikoa ya baridi, kengele za kufunga kitandani zinakuwa na milio kumfanya achezee au kusikia pindi akiamka,chandarua na hata kitanda cha mtoto.

 

 • image

  Vifaa vya kuogea kama mabeseni, sabuni ya kuogea, taulo ,seti ya kitana na nelkata, kitana kwa mtoto.

 

 •  Kiti cha kukaa cha mtoto, bembea, baby walker na nyinginezo ingawa hizi mara nyingi huwa na gharama .

 

image

 • Monitor baby –  inatatumika kusikilizia  mtoto akiwa amelazwa chumbani peke yake itamrecord sauti iwapo ataamka au kulia na mzazi atasikia monitor baby zinapatikana kwenye  maduka ya vitu vya watoto.

 

image

 • Kibebea mtoto (baby carrier)ambavyo vipo vya aina mbalimbali zingatia uzito, uimara na ubora wa kifaa unachonunua ili mtoto asijeanguka.

 

 • Unaweza pia nunua vitabu vya aina mbalimbali kama vyenye lailon kwa wale wachanga ili kuwapa hisia, picha za wanyama,matunda ama story

 • image

  Vyombo vya kulia mtoto kama seti ya vikombe, sahani na vijiko. Hapa unafaa kuzingatia rangi ya jinsia za mtoto.

 

 • Car seat zawadi hii inafaa zaidi kwawale wazazi wenye magari ivyo kabla ya kuinunua fikiri kama mlengwa wako anaihitaji

   image

 • Nguo za mtoto,soksi,viatu,chupa,khanga au vitenge vya mama

 

Wengine wanapenda kupeleka diapers,sabuni za kufulia ,pesa au vyakula navyo sio mbaya kwa mama ambe ashajifungua .

 

 

 

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →