Aina Za Maziwa Ya Kopo (Baby Formula) Na Matumizi Yake

Maziwa ya kopo (baby formula) ni maziwa ya ngo’mbe wana ya process na kuweka kwenye mfumo wa powder,na kuongezea virutubisho vingine.Maziwa ya kopo  yana utofauti sana na maziwa ya mama sababu maziwa ya mama yanavirutubisho vingi  ni asilia vinavyo mpa mtoto kinga mwilini na kumwongezea uzito mtoto kwa haraka ,wakati maziwa ya kopo yanachukua mda kumkuza mtoto na kumpa kinga ndogo mwilini na kumfunga choo.

 

 

sababu zitakazo pelekea mtoto kupewa maziwa ya kopo?

  • Mama kutokuwa na maziwa ya kutosha

  • Mtoto kutokushiba maziwa ya mama(hayamtoshi)

  • Mama kupatwa dharura (kupata safari ya mda mrefu,kuumwa au kifo n.k)

Wazazi wengi wanakosea  kuwapa watoto maziwa ya kopo kusipo sababu maalum,mtoto anatakiwa apewe maziwa ya kobo iwapo kuna sababu malum na ushauriane na daktari, lasivyo ni vizuri mtoto anyonyeshwe  maziwa ya mama ili apate virutubisho na kinga mwilini vitakavyo mwepusha na maradhi.

Aina za maziwa ya kopo 

Kuna aina nyingi za maziwa ya kopo ya watoto ,kuna mengine yalishapigwa marufuku nchini Tanzania kama (lactogen n.k)ila kuna baadhi yanatumika na ni mazuri kama

:Nan,

:Sma kopo la gold

:S26 kopo la gold

:Baby infant

:Cow gates

:Aptamil

:Similac

 

MADHARA YA MAZIWA YA KOPO

Maziwa ya kopo ni hatari sana kwa watoto sababu uaminifu ni mdogo ,kwa mfano Tanzania wafanya biashara baadhi yao sio waaminifu  wanauza maziwa fake kwa kujali maslai yao na selikali inatoa onyo mara kwa mara,mzazi unatakiwa kuwa makini sana maziwa fake huadhiri ini,figo ,kuhara,kutapika,kupata rashes,maumivu ya tumbo au kupata cancer .

USHAURI TOKA AFYA BORA KWA MTOTO

1:Maziwa ya kobo ukifungua kutumia unatakiwa utumie kwa siku 30 zaidi  hapo hayafai tena kutumika mwaga.

2:Chemsha maji ya kutengenezea maziwa kabla hujachanganya na maziwa.

3:Hifadhi maziwa kwenye chombo cha plastic chenye mfuniko hakikisha hewa haipiti.Na kwa kopo la maziwa yenye material ya steel(bati) ni sumu mbaya huchochea kupata cancer kwa urahisi kuna package mpya zipo siku hizi za material ya box nunua hizo.

 

4:Unachotakiwa nunua maziwa yalio pakiwa kwenye makopo ya plastic  au box dogo hayo ni mazuri zaidi  kama cow gate,sma n.k haya yatatoka nchini Uingereza unaweza wasiliana na huyu anayo (0787740119)

 

5: Soma expiry date(siku ya mwisho maziwa kutumika) ni hatari sana,usimpe mtoto bila kusoma tarehe.

 

6:Yakague maziwa kwa kuweka kwenye chombo cha plastik mara nyingine yanakuja na uchafu ndani mende,pini n.k kama nilivyosema kuna maziwa fake na huwa hawafatilii usafi.

 

7:Maziwa mengine huwa yanakataa watoto wanapata maumivu ya tumbo wengine hutapika hivyo unaweza mbadilishia na kumpa Aina nyingine.

 

8:Nawa mikono yako kwa maji safi kabla hujamtengenezea maziwa mtoto

 

9:Maziwa ya mama ni muhimu kuliko ya kopo au ya ng’ombe ,ya mama yanamfanya mtoto  anakuwa na kinga kubwa mwilini  ni salama zaidi kwa afya yake na hayana gharama.

Please follow and like us:
error0

About afyaborakwamtoto

Hii ni Blog maalumu inayotoa elimu juu ya mambo ya uzazi na malezi bora kwa mtoto.

View all posts by afyaborakwamtoto →